" Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo & Mitazamo ya wengine. Mchango wako katika kazi yoyote ulenge kujenga jamii yenye Kujitambua, Kujithamini na Kujiwajibisha "

 
Thursday, May 04, 2006

http://photos1.blogger.com/blogger/1437/2856/1600/DSCF0074.jpg

 Adiy: Tunataka Serikali ya Z’baritamke Muungano huu ni batili

Hey comrades

Hii ni makala iliyotoka kwenye gazeti la Mwananchi Mei 3, huu ni mwendelezo wa makala zangu kuhusu Muungano na matatizo yake. Kwa wale ambao hawakubahatika kuisoma makala hii kwenye gazeti, i would like to share it with you here! Welcome!

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kudumu kwa miaka 42, hivi sasa wametokea watu wanaohoji uhalali wa kuwapo kwake. Katika makala hii Mwandishi HAWRA SHAMTE anazungumza na Rashid Salum Adiy mmoja wa Wazanzibari 10 waliopeleka madai mahakamani wakitaka waonyeshwe hati ya asili ya makubaliano ya Muungano.

Rashid Salum Adiy na wenzake tisa walipeleka mahakamani ombi la kupatiwa taarifa yenye maelezo ya kisheria kuhusiana na kuwapo kwa itifaki ya Muungano kati ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Adiy na wenzake walifungua madai namba 20/05 katika Mahakama Kuu Zanzibar dhidi ya Mwanasheria Mkuu. Kabla ya dai hilo kupelekwa mahakamani, Juni 20, 2005 Adiy na wenzake walimpelekea barua Mwanasheria Mkuu wakitaka wapatiwe nakala ya hati ya mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar barua ambayo Mwanasheria Mkuu aliijibu Juni 22 kwa kusema kuwa ofisi yake haikuweka kumbukumbu ya nakala ya Hati ya Mkataba wa Asili wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Adiy anasema Mwanasheria Mkuu amethibitisha kwamba hakuna Mkataba wa Muungano kati ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar uliofikiwa kwa mujibu wa sheria.

Hivyo Adiy na wenzake wamefungua upya madai yao Mahakama Kuu wakiwashtaki watu watano. Wa kwanza ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakimtaka atamke kwamba Muungano si halali kwa mujibu wa sheria za mikataba ya kimataifa. Adiy anasema Mkataba wa Muungano haukufuata mkondo wa kisheria.

“Ili mkataba wa kuunganisha nchi ufikiwe ni lazima kwanza vyombo halali vya kisheria vya nchi zinazotaka kuungana vijadili suala hilo, lakini kwa upande wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Bunge la Tanganyika tu ndilo lililoketi na kupitisha Mkataba wa Makubaliano (Memorandum of Understanding),” anaeleza Adiy.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo Bunge la Tanganyika lilipitisha muswada wa makubaliano ya Muungano Aprili 25, 1964 wakati Rais wa Tanganyika Julius Nyerere na Rais wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar, Abeid Aman Karume waliweka saini makubaliano hayo ikiwa ni pamoja na vipengele 11 vya mambo ya Muungano, Aprili 22, 1964.

Adiy anasema mkataba wa Muungano haukupaswa kufungwa kabla ya ‘Memorandum of Understanding,’ na hilo ni kosa kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa.

Hata hivyo Adiy anasema ikiwa Bunge la Tanganyika liliketi na kuridhia makubaliano ya Muungano, Baraza la Mapinduzi Zanzibar halikuketi kuridhia makubaliano hayo. “Ikiwa wanasema kuwa kwa wakati ule Zanzibar ilikuwa ikiendeshwa kwa ‘decree’ ya kijeshi, basi ielezwe bayana kwamba, Muungano uliopo uliundwa kwa amri za kijeshi chini ya Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Tanganyika na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na ikiwa hivyo ndivyo, basi Muungano uliopo hauna ridhaa ya wananchi ni muungano wa kijeshi.

“Unajua hakuna Muungano uliofanyika, bali uliofanyika ni uvamizi tu na hivi sasa Zanzibar ni koloni la Tanganyika.

“Sisi tunachotaka ni kuonyeshwa mkataba wa Muungano ambao uliwekwa saini na Nyerere na Karume na tumeambiwa kuwa haupo, na tumeambiwa hivyo kwa sababu hakuna kilichosainiwa,” anaeleza Adiy.

“Wa pili atakayeshtakiwa katika dai jipya ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi kwa sababu yeye kama Mtendaji Mkuu alipeleka indhari gani kwa serikali kuifahamisha kwamba kinachofanywa si halali?” Anahoji Adiy.

Wa tatu ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huyu anatakiwa aeleze kwanini ameiondolea Zanzibar uanachama wake wa kudumu katika Umoja wa Mataifa?

Wa nne ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa ni chama kilichoweza kuweka sera na misingi ya kisiasa iliyoikandamiza na kuidhoofisha Zanzibar.

Na wa mwisho atakayeburuzwa mahakamani ni Spika wa Baraza la Wawakilishi ambaye yeye atahojiwa kwanini amesimamia vikao vya Baraza bila kutaka kuthibitishiwa kwamba Zanzibar ni sehemu ya Muungano na anapaswa awe na maandishi ya makubaliano yaliyofikiwa.

Adiy anasema ikiwa Mwanasheria Mkuu atashindwa kutamka kuwa Muungano si halali kwa mujibu wa sheria, basi yeye na wenzake watawaeleza wananchi kuhusu jambo hilo na hatimaye ni nguvu ya umma ndiyo itakayoamua la kufanya.

“Sisi wasimamizi wa suala hili tuko 10 tu ambao ni mimi Adiy na wenzangu ni Rashid Ahmed Rashid, Rashid Yussuf Mchenga, Haji Sheha Hamadi, Abdallah Hassan Mrisho, Mbaruk Sheha Simai, Khamis Ismail Makame , Ali Simai Mwadini, Nassor Hassan Nassor na Ali Omar Ali, lakini nyuma yetu wake Wazanzibar zaidi ya 10,000 wanaotuunga mkono, hivyo tutahakikisha kwamba dai letu hili ikikosa majibu ya kisheria ya kuridhisha, tutawahamasisha Wazanzibari wengi zaidi watuunge mkono na hatimaye iitishwe kura ya maoni, kinyume cha hivyo hatutapumzika mpaka tujue khatima ya Zanzibar chini ya uvamizi wa Tanganyika.

“Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inasema kuwa, Zanzibar ni sehemu ya Muungano wa Tanzania, ikiwa hivyo ndivyo Tanzania iko wapi ikiwa walioungana ni Tanganyika na Zanzibar?” Anahoji Adiy.

Adiy na wenzake, Aprili 26, 2006 wamefanikiwa kufungua kesi mpya ya madai katika mahakama kuu, kesi hiyo ya madai nambari 04/06 linaloiomba mahakama itoe amri ya ‘CERTIORARI NA MANDAMUS’ ili kumlazimisha Mwanasheria Mkuu atamke kwamba Muungano si halali kwa mujibu wa sheria za mikataba ya Kimataifa.

Miongoni mwa mashtaka anayoshtakiwa Mwanasheria Mkuu Zanzibar ni kukataa kutoa tamko la ukweli la kisheria kwamba Muungano kati ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika sio halali na Zanzibar si sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kadhalika Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi anashtakiwa kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu Zanzibar kufanya kitendo kinyume cha sheria na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la mwaka 2003 kwa kuidanganya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na wananchi wa Zanzibar kuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar imeungana na Jamhuri ya Tanganyika na kuwa Jamhuri moja huru.

Suala jingine wameliita kuwa ni kufanyiwa udanganyifu na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na dola ya kigeni ya Tanganyika na kuvunjwa kwa haki mbalimbali za Zanzibar kwa Wazanzibari kupotezewa uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyenwe ndani na nje ya nchi yao kwa muda wa miaka 42.

KUHUSU MIMI

JINA:Hawra Shamte
MAKAZI:Dar es salaam
NCHI:Tanzania
KAZI:Mwandishi

KUELEKEA BUNGE LA BAJETI 2006

QuickTopic free message boards
Bonyeza hapa ili uweze kuelezea: NINI MTAZAMO WAKO JUU YA BAJETI IJAYO YA MWAKA 2006/07 NCHINI TANZANIA?

VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI

  • The Citizen
  • Mwananchi
  • Mwanaspoti
  • Business Times
  • Majira
  • Daily News
  • Nipashe
  • The Guardian
  • The Express
  • Kiongozi
  • Uhuru/Mzalendo
  • Arusha Times
  • BLOGI ZA KISWAHILI

  • Bangaiza
  • Mwandani
  • Pambazuko
  • Damija
  • Mtafiti
  • Martha
  • Gaphiz
  • Swahili time
  • Miruko
  • Dira yangu
  • Msangimdogo
  • Jeff Msangi
  • Kasri la mwanazuoni
  • Kurunzi
  • Baragumu
  • Mawazohuru
  • Fikra Thabiti
  • Mtandaoni
  • Motowaka
  • Mkwinda
  • Ngurumo
  • Nyembo
  • Bwaya
  • Omega
  • Tafakari za Maisha
  • Nuru akilini
  • Mtandawazi
  • Mhujumu
  • Vijimamboz
  • Wakati wa Ukombozi
  • Kijiwe Joto
  • Watoto Wetu
  • Jungu kuu
  • Kisima cha Weledi
  • Jarida la Ughaibuni
  • Bhalezee
  • Sauti ya Baragumu
  • Kona yangu
  • Furahia Maisha
  • Bakanja
  • Terrie Swai
  • Fatma Karama
  • Kazonta
  • Binti Afrika
  • Blogu ya Kilimo
  • Ukombozi
  • Mwafrika
  • Digital Africa
  • Blogu ya lugha mseto
  • BLOGI ZA WAAFRIKA

  • BLOGAFRICA
  • BLOGU ZA WAAFRIKA
  • DIGITAL AFRICA
  • MAMA JUNKYARD'S
  • MSHAIRI
  • KENYAN PUNDIT
  • MONGI DREAMS
  • ISARIA MWENDE
  • CUNNING LINGUISTICA
  • ETHIOPUNDIT
  • MOCHALICIOUS
  • UNGANISHA
  • DEMOKRASIA KENYA
  • CHANUKA
  • BANKELE
  • MAARIFA/AKIEY
  • AFROMUSING
  • NEHANDA DREAMS
  • BLACK LOOKS
  • YUMMY WAKAME
  • AFRICAN OIL POLITICS
  • NUBIAN SOUL
  • SANAA
  • VIRTUAL INSANITY
  • MENTAL ACROBATICS
  • KENYA UNLIMITED
  • JIKUMBUSHE KAZI ZANGU ZA ZAMANI

    April 2006 May 2006 June 2006 October 2007 November 2007 December 2007 May 2008 July 2008 October 2008 July 2009 August 2012 October 2012

    Imetengenezwa na

    Ukibofya hapa utapelekwa katika Blogi ya msangimdogo

    na inawezeshwa na