" Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo & Mitazamo ya wengine. Mchango wako katika kazi yoyote ulenge kujenga jamii yenye Kujitambua, Kujithamini na Kujiwajibisha "

 
Wednesday, December 05, 2007

 Rais anza kazi, nasi tutakusaidia kukomesha ufisadi huu

KUKEMEA au kukaripia kwa kawaida ni tabia ya wakubwa, wenye mamlaka, wawe katika ngazi ya kaya, tarafa, kijiji, wilaya, mkoa hadi taifa.

Rais anapo kemea au anapo onya huwa anafanya wajibu wake, anafikiri kwamba kwa kufanya hivyo kuna watu watamsikiliza kwa sababu karipio la Rais ni amri ya katazo.

Wanaofuatilia historia ya nchi hii watagundua kuwa ni katika awamu ya kwanza tu ya serikali zote mbili (ile ya Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Karume), ndipo makemeo na makaripio yalipokuwa yakifanya kazi zake ipasavyo. Linapotamkwa tu, hutekelezwa, hadi ikafikia watu kukamatwa na kuwekwa jela kwa kosa la uhujumu wa uchumi wakati hata hiyo sheria ya uhujumu wa uchumi ikiwa bado haijatungwa.

Wakati ule Watanzania bado walikuwa waoga, walikuwa wanagenzi, ndio kwanza wanajifunza, walizoea kutawaliwa na kuamriwa. Hizo zilikuwa ndio zama za ‘zidumu fikra za Mwenyekiti.’

Katika zama hizi, mambo yamebadilika, watu hawashtushwi tena na makemeo, makaripio na maonyo. Kauli za kisiasa kwao si tatizo, kwani si wamezoea kuzisikia? Je kwani huo si sawa na wimbo wa taifa, hata mtu akiwa usingizini akili yake inauimba?

Rais Jakaya Kikwete akiwa mkoani Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita, alitoa tahadhari kwa viongozi wanaojigawia miradi ya wananchi maskini kuwa wasipoacha tabia hiyo watakiona cha mtema kuni.

Alipokuwa mkoani Tabora wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Rais pia alitumia fursa hiyo kutoa onyo, aliwakemea wanaoeneza virusi vya ukimwi kwa makusudi kuwa watakiona cha moto.

Rais aliwahi kutoa tahadhari kwa wala rushwa na kuwaambia kuwa majina yao anayo ila anawapa muda wajirekebishe.

Katika kanuni za uongozi hasa wa nchi, mara nyingine si vizuri sana kufikiri kwamba unaweza kuibadilisha jamii kwa kutoa tahadhari, onyo, karipio au kemeo. Mara nyingine uongozi unahitaji vitendo zaidi kuliko maneno. Kama Rais alivyowahi kusema kuwa kelele za wapinzani amezizoea, hivyo naye anapaswa ajihadhari ili ‘kelele’ zake nazo zisije zikazoeleka.

Kuna mambo ambayo viongozi wanapaswa wayatende bila kusema, wanaweza kumuadhibu mtu kwa kosa la uhujumu uchumi au kuhujumu miradi, kimya kimya na ujumbe ukafika. Binafsi naona si vema kwa Rais kupenda kutoa maonyo majukwaani kwani tunachoshindwa Watanzania ni kufanya kweli na kamwe si kusema.

Kuna maonyo na maelekezo yaliyotolewa Ngurdoto kwa viongozi wa Serikali, kwa kiasi gani maonyo yale yameleta athari? Je maelekezo yale waliyoyapata viongozi wetu katika semina elekezi hayakuweza kubadilisha muundo na mtindo wa uongozi serikalini? Je ni kwa kiasi gani Serikali hii imekwenda kwa wananchi na imekuwa kweli Serikali ya watu?

Hata hivyo alilolizungumza Rais ni dhahir, nami nachukua nafasi hii kumuunga mkono. Si vibaya kutoa tahadhari na karipio lakini isiwe ndiyo mazoea. Hili la viongozi kujipendelea, angalau Rais ameligundua na nashukuru amelizungumzia. Je ni miradi mingapi ambayo walengwa wake ni wananchi wa kipato cha chini ambayo huchukuliwa na wakubwa? Rais amezungumzia mradi wa ugawaji wa miche ya miembe inayozaa kwa muda mfupi, lakini pia upo mradi wa usambazaji mbolea kwa wakulima, je ni wakulima wangapi wadogo wanaofaidika na mbolea hiyo?

Kuna mradi wa upimaji viwanja katika maeneo mapya, je ni wananchi wangapi walalahoi wanaovipata viwanja hivyo? Je hatuwaoni wakubwa jinsi wanavyojikatia eka kwa eka, eti ardhi ni mali hivyo wanaweka akiba? Je hawa ‘pangupakavu’ wanawezeshwa vipi nao kujipatia angalau ekari moja moja ya akiba?

Kuna nafasi za masomo zinazotolewa kwa ajili ya watoto wa wakulima na wafanyakazi, wavuja jasho wa nchi hii, je ni watoto wa wavuja jasho wangapi wanaopata fursa hizo?

Kuna mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu iliyokusudiwa kwa ajili ya wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo, je ni watoto wa vigogo na matajiri wangapi wanaopata mikopo hii ambayo hawastahili kuipata?

Ipo miradi ya Tasaf na Mkukuta, je viongozi wanajilinda vipi na ulafi na uchoyo ili miradi hiyo iwafikie walengwa? Ni vipi Tanzania itatimiza malengo ya millennia ya kupunguza umaskini uliokithiri wa asilimia 50 ya wananchi wake, ikiwa kumbe wapo viongozi walafi, waroho, wanaojilimbikizia na kupora miradi ya wananchi?

Kuna miradi ya usambazaji maji, katika hili nalo wako wahujumu wanaounganisha mabomba katikati ya bomba kubwa la usambazaji na kuyavuta kwa ‘pump’ hivyo kusababisha wengine kuyakosa, je hawa nao wanachukuliwa hatua gani?

Rais unapaswa upange mikakati madhubuti ya kuwachukulia hatua kali hawa wasiopeleka miradi kwa walengwa na badala yake kujinufaisha wao binafsi kutokana na nafasi walizonazo.

Ukisikia ufisadi, huu wa kiongozi kuwa ‘mwamba ngoma, ngozi kuvutia kwake,’ ndio ufisadi mkubwa. Rais anza kazi, nasi tuko nyuma yako, tutakusaidia kukomesha ufisadi huu.

Mwandishi ni Mhariri wa Siasa wa gazeti la Mwananchi.
hshamte@mwananchi.co.tz

KUHUSU MIMI

JINA:Hawra Shamte
MAKAZI:Dar es salaam
NCHI:Tanzania
KAZI:Mwandishi

KUELEKEA BUNGE LA BAJETI 2006

QuickTopic free message boards
Bonyeza hapa ili uweze kuelezea: NINI MTAZAMO WAKO JUU YA BAJETI IJAYO YA MWAKA 2006/07 NCHINI TANZANIA?

VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI

 • The Citizen
 • Mwananchi
 • Mwanaspoti
 • Business Times
 • Majira
 • Daily News
 • Nipashe
 • The Guardian
 • The Express
 • Kiongozi
 • Uhuru/Mzalendo
 • Arusha Times
 • BLOGI ZA KISWAHILI

 • Bangaiza
 • Mwandani
 • Pambazuko
 • Damija
 • Mtafiti
 • Martha
 • Gaphiz
 • Swahili time
 • Miruko
 • Dira yangu
 • Msangimdogo
 • Jeff Msangi
 • Kasri la mwanazuoni
 • Kurunzi
 • Baragumu
 • Mawazohuru
 • Fikra Thabiti
 • Mtandaoni
 • Motowaka
 • Mkwinda
 • Ngurumo
 • Nyembo
 • Bwaya
 • Omega
 • Tafakari za Maisha
 • Nuru akilini
 • Mtandawazi
 • Mhujumu
 • Vijimamboz
 • Wakati wa Ukombozi
 • Kijiwe Joto
 • Watoto Wetu
 • Jungu kuu
 • Kisima cha Weledi
 • Jarida la Ughaibuni
 • Bhalezee
 • Sauti ya Baragumu
 • Kona yangu
 • Furahia Maisha
 • Bakanja
 • Terrie Swai
 • Fatma Karama
 • Kazonta
 • Binti Afrika
 • Blogu ya Kilimo
 • Ukombozi
 • Mwafrika
 • Digital Africa
 • Blogu ya lugha mseto
 • BLOGI ZA WAAFRIKA

 • BLOGAFRICA
 • BLOGU ZA WAAFRIKA
 • DIGITAL AFRICA
 • MAMA JUNKYARD'S
 • MSHAIRI
 • KENYAN PUNDIT
 • MONGI DREAMS
 • ISARIA MWENDE
 • CUNNING LINGUISTICA
 • ETHIOPUNDIT
 • MOCHALICIOUS
 • UNGANISHA
 • DEMOKRASIA KENYA
 • CHANUKA
 • BANKELE
 • MAARIFA/AKIEY
 • AFROMUSING
 • NEHANDA DREAMS
 • BLACK LOOKS
 • YUMMY WAKAME
 • AFRICAN OIL POLITICS
 • NUBIAN SOUL
 • SANAA
 • VIRTUAL INSANITY
 • MENTAL ACROBATICS
 • KENYA UNLIMITED
 • JIKUMBUSHE KAZI ZANGU ZA ZAMANI

  April 2006 May 2006 June 2006 October 2007 November 2007 December 2007 May 2008 July 2008 October 2008 July 2009 August 2012 October 2012

  Imetengenezwa na

  Ukibofya hapa utapelekwa katika Blogi ya msangimdogo

  na inawezeshwa na